• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

TARURA Namtumbo yaendelea kufungua barabara mpya

Imewekwa kuanzia tarehe: June 6th, 2023

WAKALA wa barabara za mijini na vijijini(Tarura)wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma,imeanza kazi ya kufungua barabara mpya katika maeneo mbalimbali wilayani humo ili kuchochea kasi ya maendeleo na ukuaji wa uchumi wa wananchi.

Miongoni mwa barabara mpya zilizofunguliwa ni Mandepwende- Masuguru yenye urefu wa kilomita 15 kwa gharama ya Sh.milioni 69 ambayo  imepita katika maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa mazao ya kilimo na biashara.

Kaimu meneja wa Tarura wilayani Namtumbo Mhandisi Albert Mtimba alisema,kabla ya kufunguliwa kwa barabara hiyo wananchi wa maeneo hayo walipata shida kubwa ya kusafirishaji mazao kwenda sokoni.Kwa mujibu wa Mtimba ni kwamba,hali hiyo iliwaathiri sana wananchi wa maeneo hayo katika jitihada zao za kujikomboa na umaskini kwa kuwa walilazima kuuza mazao yakiwa shambani tena kwa bei ndogo ili kuepuka gharama ya usafirishaji.

Alisema,awali haikuwepo barabara ya uhakika inayounganisha kata ya Rwinga na Masuguru kwa kutumia vyombo vya moto kama magari na pikipiki,badala yake wananchi walilazimika kutembea kwa miguu wanapohitaji kwenda katika maeneo mengine kufuata huduma za kijamii.

Alisema,kutokana na jitihada za Tarura kwa sasa barabara hiyo inapitika na imeanza kutumika kusafirisha mazao na kuwataka wananchi kuitumia kwa ajili ya shughuli  mbalimbali za maendeleo.

Mkazi wa kijiji cha Masuguru Hamis Undole alisema,awali barabara hiyo ilikuwa changamoto kubwa pindi wanapotaka kusafiri kwenda maeneo mengine kufuata huduma mbalimbali za kijamii.

Undole,ameishukuru serikali ya awamu ya sita kupitia wakala wa barabara za mijini na vijijini Tarura kufungua barabara mpya inayounganisha maeneo yenye uzalishaji na masoko.

Mwanahidi Abbas mkazi wa kata ya Rwinga alisema,awali barabara hiyo ilikuwa na mashimo mengi na wakati wa masika haikuweza kupitika kwa urahisi kutokana na mashimo yaliyokuwepo katikati ya barabara kujaa maji na hivyo kusababisha kero kubwa.

Alisema,kwa sasa barabara hiyo ni  ni rafiki na wameanza kuitumia katika shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kusafirisha mazao ya kilimo.

Abbas,ameipongeza serikali kwa kazi nzuri iliyofanya kufungua barabara hiyo ambayo itasaidia  sana kuharakisha maendeleo yao na kukua kwa uchumi wa wilaya ya Namtumbo.

Matangazo

  • RATIBA ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 October 14, 2023
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara December 31, 2023
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma September 30, 2023
  • WALIOCHAGULIWA kidato cha kwanza March 31, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatangaza kufunga rasmi mfumo wa ununuzi wa TANePs Septemba 30 mwaka huu

    September 23, 2023
  • MKUU wa Mkoa alivyomkabidhi Mkakati wa Utalii Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma

    September 23, 2023
  • CHIFU wa Wangoni alivyokabidhiwa Mkakati wa Utalii Mkoa wa Ruvuma

    September 23, 2023
  • MKUU wa Wilaya ya Tunduru azindua Jukwaa la Wanawake wa Tunduru

    September 23, 2023
  • Tazama zote

Video

WAZIRI APONGEZA UWEKEZAJI MKUBWA HALMASHAURI YA MADABA
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: 0252602256

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.