Timu ya Menejimenti ya Sekretarieti ya Mkoa wa Ruvuma, ikiongozwa na Joel Mbewa, Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa, imekagua miradi minne ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 875 katika Halmashauri ya Madaba, Wilaya ya Songea.
Moja ya miradi iliyokaguliwa ni ujenzi wa stendi ya mabasi ya Madaba unaogharimu shilingi milioni milioni 205.
Kutokana na kubanwa na ratiba ililazimika Menejimenti hiyo kukagua baadhi ya miradi usiku ukiwemo mradi wa ujenzi wa mabweni katika sekondari ya Madaba na ujenzi wa stendi ya mabasi Madaba.
Mbewa amewapongeza wataalam kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo huku akisisitiza kasi na ubora katika miradi inaendelea kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa tija na miradi inaleta matokeo chanya kwa wananchi.
Timu hiyo inaendelea leo, Novemba 7, 2025, na ziara ya ufuatiliaji katika miradi mingine ya maendeleo ndani ya Halmashauri ya Madaba.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.