Katika hatua ya kipekee ya upendo na mshikamano wa kijamii, Meneja Msaidizi wa Ukaguzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Ruvuma, Mabula Mayiku, ameongoza zoezi la kukabidhi msaada wenye thamani ya shilingi milioni 3 kwa wagonjwa wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songea.
Hatua hii ni sehemu ya utamaduni wa kila mwisho wa mwaka wa fedha, ambapo TRA Ruvuma hurudisha shukrani kwa wananchi wakiwemo walipa kodi ambao mchango wao unawawezesha kufanikisha majukumu ya kila siku.
Msaada huo umejumuisha mashuka, sukari, unga, mafuta, mchele, pamoja na vifaa vya usafi kama pipa la taka na fagio.
“Tumekuja na zawadi hizi si kwa sababu tuna ziada, bali kwa sababu tunatambua mchango wa walipa kodi katika maendeleo ya taifa letu. Leo tupo hapa kuwapa faraja wagonjwa na kuhakikisha mazingira yao yanabaki safi na yenye utu,” amesema Mayiku.
Akitoa neno la shukrani, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Magafu Majura, amesisitiza kuwa msaada huu utaleta athari chanya kwa wagonjwa, wakiwemo walipa kodi wanaopata matibabu.
“Tunaamini kwamba kwa msaada huu, wagonjwa wetu watapata nafuu haraka, kurudi kwenye kazi zao, na kuendelea kushiriki katika maendeleo ya taifa kupitia ulipaji wa kodi,” amesema Dkt. Majura kwa furaha.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.