Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewataka Wakulima mkoani Ruvuma kuanza kununua mbolea mapema kwa ajili ya kujianda na msimu mwingine wakilimo
Hayo ameyasema hivi karibuni katika kongamano la kilimo biashara ambalo liliwakutanisha Wakulima wa Mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kuwabadilisha kuacha kufanya kilimo mazoea na badala yake kulima kilimo chenye tija.
“Kupitia kongamano hili nawaomba Wananchi na Wakulima wote wa Mkoa wa Ruvuma twendeni tunune mbolea kipindi hiki tusisubiri hadi mvua zianze ndipo tuanze kupanga foleni na kwa taarifa nilizo nazo mbolea imekuja kwa wingi katika Mkoa wetu wa Ruvuma”
Aidha, Kanali Thomas amewataka wakulima kufanya kulimo mkakati kwa kulima mazao mengine ya biashara ili kuweza kujiongezae kipato.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.