• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

UBAKAJI bado ni tatizo kwa watoto nchini

Imewekwa kuanzia tarehe: May 9th, 2020

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametoa takwimu za ukatili wa kijinsia kwa watoto huku akitaja ubakaji kuongoza kutokana na kuongezeka kila mwaka.

Waziri Ummy ametoa majibu hayo kwa njia ya maandishi akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Catherine Ruge (Chadema), aliyetaka kujua mkakati wa serikali kudhibiti ubakaji.

“Kumekuwa na ongezeko kubwa la vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani ulawiti na ubakaji kwa wanafunzi vinavyofanywa baina ya wanafunzi wenyewe kwa wenyewe au watu wa karibu katika familia, je, serikali ina mkakati gani wa dharura kudhibiti matendo hayo?,” ameohoji.

Akijibu swali hilo Ummy amesema tatizo la ukatili wa kijinsia kwa watoto bado ni kubwa ambapo Takwimu za Jeshi la Polisi zinaonyesha kuongezeka kwa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ambapo mwaka 2017 matukio yalikuwa 13,457, mwaka 2018 matukio 14,419 na mwaka 2019 matukio 15,680.

“Aidha, kwa mwaka 2019 vitendo vya ukatili vilivyoongoza ni Ubakaji (6,506), mimba za wanafunzi (2,830) na Ulawiti (1,405).

“Mikakati ya serikali katika kukabiliana na ulawiti pamoja na ubakaji ni kutoa elimu kwa jamii kupitia watu mashuhuri, viongozi wa kisiasa, dini na mila ili kushiriki katika kubadilisha tabia na mienendo ya baadhi ya watu wanaoendeleza tabia za aina hiyo katika jamii kwa kuchukua hatua kali za kisheria kuwafikisha mahakamani wale wote wanaotenda makosa hayo ili haki itendeke kwa mujibu wa Sheria.

“Pia kuna huduma za simu bila malipo kwa watoto ambayo inawezesha jamii kutoa taarifa za vitendo vya ukatili,” amesema.

CHANZO MTANZANIA DIGITAL MEI7,2020

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara June 30, 2023
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma September 30, 2023
  • WALIOCHAGULIWA kidato cha kwanza March 31, 2023
  • UTARATIBU wa kupandisha hadhi barabara June 30, 2023
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KAMATI ya Siasa Ruvuma yakagua jengo la DED Mbinga

    February 08, 2023
  • MAKITA sekondari wamshukuru Rais Samia kuwajengea madarasa

    February 08, 2023
  • TARURA yatumia bilioni moja kujenga lami Mbinga

    February 08, 2023
  • NDEGE mwenye uwezo wa kusafiri Dunia nzima humpumzika ndani ya hifadhi ya Gesimasowa Ruvuma

    February 08, 2023
  • Tazama zote

Video

BARABARA ya Songea -Msumbiji kuanza kujengwa
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 74 Songea

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: 0252602256

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.