I Mahali alipoadhimisha Misa Baba Mtakatifu Hayati Papa Yohane Paulo wa Pili mwaka 1990, leo panang’aa kwa tumaini jipya kupitia Shule ya Msingi ya Elimu Maalum St. Vincenti, katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, shule ya bweni inayobadilisha maisha ya watoto wenye ulemavu wa kusikia na kuthibitisha kuwa ulemavu si mwisho wa ndoto.
Ilianzishwa Februari 2, 1992 na Kanisa Katoliki kwa ushirikiano na Serikali baada ya kubainika kuwa watoto wengi viziwi ukanda wa Kusini walikosa fursa ya elimu. Mwaka 2000, shule ilitunukiwa Cheti cha Ubora wa Taifa kutokana na matokeo bora ya kitaaluma.
Shule ina rekodi imara ya ufaulu kwa asilimia 100 kwa darasa la nne na Darasa la saba lMkuu wa shule, Sr. Malieta Mlelwa, anasema dira yao ni “Elimu, Usafi na Kazi,” wakihakikisha kila mtoto anapata nafasi sawa.
Mbali na masomo ya kawaida, wanafunzi hupata mafunzo ya ufundi, teknolojia na kompyuta, wakihitimu na vyeti vya VETA vinavyowaandaa kujitegemea..
Jamii inahimizwa kuacha kuwaficha watoto wenye ulemavu kwa sababu wakipewa elimu, hugeuka kuwa nguvu ya maendeleo. St. Vincenti si shule tu; ni urithi wa historia, alama ya usawa na mwanga wa kesho ya Tanzania jumuishi.
Kama una mtoto kiziwi miaka 5 hadi 6 wasiliana nasi Mkuu wa shule simu 0763374500/0624026120, mariethasr1998@gmail .com
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.