Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, mkoani Ruvuma Mhe. Kisare Makori, amehitimisha rasmi mafunzo ya Jeshi la Akiba (Mgambo) yaliyodumu kwa miezi minne katika Kijiji cha Kitura.
Katika hotuba yake, Mhe. Makori aliipongeza Ofisi ya Mshauri wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Mbinga kwa kusimamia mafunzo hayo kwa ufanisi, huku akiwashukuru wahitimu kwa nidhamu, mshikamano na uzalendo waliouonesha.
Aidha, amewataka vijana hao kutumia maarifa waliyopata kuimarisha maendeleo na ustawi wa jamii, na sio kushiriki vitendo vya kihalifu.
Kwa upande wake, Meja Izack Mugomba, Mshauri wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Mbinga, alisema jumla ya vijana 54 wamehitimu mafunzo hayo, akisisitiza kuwa mshikamano wa wananchi wa Kijiji cha Kitura umechangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha mafunzo hayo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.