Viongozi wa dini mkoani Ruvuma wameungana kutoa wito wa amani na utulivu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, wakisisitiza kuwa amani ni urithi mkubwa kuliko neema nyingine yoyote.
Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Ramadhan Mwakilima, alisema viongozi wa dini wana jukumu la kuhakikisha jamii inadumisha usalama, haki na uadilifu.
“Amani ikipotea, hakuna ucha Mungu, hakuna maendeleo, hakuna mafanikio,” alisema Shekhe Mwakilima.
Kwa upande wake, Mchungaji Alukwin Kapinga wa Kanisa la Biblia Mahenge aliwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura, akisema ni haki yao ya kikatiba na wajibu wa kiraia.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.