Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imeendesha mafunzo maalum kwa wahudumu wa vituo vya afya vya Serikali na binafsi katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga, ikiwa ni maandalizi ya uboreshaji wa huduma za bima ya afya kuanzia Januari 2026.
Mafunzo hayo yametolewa na Meneja wa Kanda ya Kusini wa TIRA, Bw. Salim Iyungwa, akishirikiana na Afisa Bima Mkuu wa Kanda ya Kusini, Bw. Fabian Mbegeta.
Lengo ni kuwajengea uwezo wahudumu wa afya kuhusu usajili wa bima, matumizi ya mifumo ya bima ya afya na utoaji wa huduma bora kwa wanufaika wa bima wanapofika vituoni.
Hatua hii inalenga kuongeza ufanisi, uwazi na huduma zenye viwango bora kwa wananchi wote.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.