baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri kutoka Mkoa wa Ruvuma wametembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga katika Viwanja vya Maonesho ya Nane Nane, John Mwakangale jijini Mbeya, wakijionea ubunifu na mafanikio katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi.
Waliotembelea banda hilo ni pamoja na Bi. Amina Seif (Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga), Bw. Sajidu Mohamed (Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba), Bi. Elizabeth Gumbo (Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea) na Bw. Khalid Khalif (Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa).
Mbali na kutembelea maonesho hayo ya kitaifa, Wakurugenzi hao pia walishiriki zoezi la kupima hali zao za lishe, wakisisitiza umuhimu wa lishe bora kwa maendeleo ya rasilimali watu katika ngazi zote.
Nane Nane 2025 – Tukutane John Mwakangale, tuyapate maarifa ya Kilimo Biashara kwa kwa vitendo
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.