Katika hatua inayochochea mageuzi ya uwazi na uwajibikaji, Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na wasaidizi wao Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga wamepatiwa mafunzo maalum ya matumizi ya Mfumo wa Manunuzi ya Umma kwa Njia ya Kielektroniki (NeST), mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.Mafunzo hayo, yaliyoendeshwa na wataalamu kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Kanda ya Kusini, yamelenga kuongeza ufanisi katika matumizi ya rasilimali za umma, kuimarisha uwazi wa zabuni na kupunguza mianya ya rushwa.Akizungumza wakati wa mafunzo, mwezeshaji ndugu Theophil Ngowi amesema PPRA inalenga kuwajengea uwezo viongozi hao kuelewa kwa kina mfumo wa NeST, hususan vipengele vipya vilivyoongezwa, pamoja na Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2023 na Kanuni zake za mwaka 2024.Kwa mujibu wa Ngowi, NeST hufanya mchakato mzima wa zabuni kuwa wazi na unaofuatilika, hivyo kupunguza malalamiko ya wazabuni. Naye Afisa Manunuzi, Bi. Eveline Mwakanyamale amesema mafunzo hayo yataongeza ubora wa huduma na kupunguza lawama kutoka kwa wateja
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.