Ghafla hali ya amani katika Kitongoji cha Likologo, Kijiji cha Wenje – Tunduru, mkoani Ruvuma imegeuka kuwa simanzi baada ya tukio la kusikitisha la mauaji ya watu watano na kujeruhi wengine watatu, kufuatia mgogoro kati ya wakulima na wafugaji usiku wa Oktoba 1, 2025.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma limethibitisha kuwashikilia watu 15 wanaodaiwa kuhusika katika tukio hilo, likiendelea na uchunguzi wa kina kuhakikisha wote waliohusika wanakabiliwa na mkono wa sheria.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, ACP Marco Chilya, ametoa rai kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake kushirikiana na viongozi wa vijiji pamoja na Jeshi la Polisi katika kutafuta suluhu za amani.
Tukio hili limeibua mjadala mpana kuhusu namna jamii inavyoweza kuimarisha mawasiliano, mshikamano na usuluhishi ili kuepusha matukio ya umwagaji damu yanayozuilika.
Je, suluhu ya kweli kati ya wakulima na wafugaji inaweza kupatikana?
#Tunduru #Ruvuma #AmaniKwanza #BreakingNews #TanzaniaNews #WakulimaNaWafugaji #StopMobJustice
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.