Kampuni ya AVIV imeonesha dhamira ya dhati ya kuwekeza kwenye kilimo cha kahawa katika Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma
Meneja wa Kilimo wa kampuni hiyo, akiwa na timu ya wataalam, amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri,ya Madaba Wakili Sajidu Idrisa Mohamed, pamoja na Mkuu wa Idara ya Kilimo kujadili mpango kabambe wa uwekezaji.
Uwekezaji huu unatarajiwa kuleta:
✅ Ajira mpya kwa wananchi
✅ Miche bora ya kahawa kwa wakulima
✅ Soko la uhakika kwa kahawa ya Madaba
✅ Uboreshaji wa huduma za jamii – afya na elimu
Madaba imefungua milango kwa wawekezaji, ikilenga kuibua fursa mpya na kuinua uchumi wa wananchi kupitia zao la kahawa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.