Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho ametembelea mradi wa maji ya mtiririko unaotekelezwa katika Kijiji cha Lipaya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma
Mheshimiwa Mhagama kwa niaba ya Viongozi na Wananchi wa Kijiji cha Lipaya Kata ya Mpitimbi ametoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za mradi huo ambazo zinaenda kutatua changamoto ya ukosefu wa maji katika kijiji cha Lipaya na vijiji jirani.
"Wito wangu kwenu ni kuendelea kuwasisitiza na kuwasihi kutunza miundombinu yote ya mradi huu wa maji ili uweze kuwanufaisha nyie na vizazi vijavyo", amesisitiza Mhe. Waziri Mhagama.
Akisoma taarifa Mhandisi wa Maji Wilaya ya Songea Triphon Mwanangwa amesema mradi huu hadi kukamilika utagharimu fedha kiasi cha zaidi ya Bilioni 1.9 kutoka Serikali Kuu.
Mhandisi Mwanangwa ameongeza kuwa chanzo cha maji kinauwezo wa kuzalisha lita milioni 3,196,800 kwa siku na mahitaji ya maji katika kijiji cha Lipaya kwa siku ni lita laki 468,123 hivyo kutakuwa na maji ya ziada ambayo yatasambazwa katika vijiji jirani.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Menas Komba amewataka wananchi kutunza mazingira kwa kupanda miti katika maeneo yao na maeneo yaliyo karibu na vyanzo vya maji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.