Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma imetembelea mradi wa Kituo cha afya Mkasale kata ya Namasakata wilaya ya Tunduru ambacho kimeanza kutoa huduma ya upasuaji baada ya serikali kutoa kiasi cha shilingi milioni 460 zilizokamilisha mradi huo na kuwaondolea kero wananchi ambao walikuwa wanasafiri umbali mrefu kutafuta huduma ambapo hadi sasa watu 51 wamefanikiwa kufanyiwa upasuaji na wote wapo salama
Mkuu w Mkoa wa Ruvuma christina mndeme amewapongeza wananchi wa kata ya Matemanga na uongozi mzima wa wilaya ya Tunduru kutumia shilingi milioni 43 kutekeleza mradi wa maji ambao serikali iliwatengea zaidi ya shilingi milioni 215
Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma imeendelea kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya ya Nyasa na kufika katika mradi wa chuo cha ufundi stadi VETA Wilaya ya Nyasa ambacho serikali imetoa shilingi bilioni mbili kutekeleza mradi
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.