KAMATI ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme imekagua kivuko cha mto Ruvuma eneo la Mitomoni na kukusudia kujenga daraja ambalo linaunganisha wilaya ya Songea na Nyasa umbali wa kilometa 140 kutoka mjini Songea.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ametembelea Kituo cha Uhamiaji cha Mkenda Songea kulichopo kilometa 140 kutoka mjini Songea eneo la mpaka wa Tanzania na Msumbiji.Mndeme alifurahishwa na kazi za ulinzi zinazofanywa na askari maalum watano wa kulinda mpaka hivyo aliamua kuwapa motisha ya shilingi laki tano nao walishukuru kwa staili ya nyakua nyakua.
TUME ya Taifa ya Uchaguzi inaendesha mazoezi mawili muhimu katika Jimbo la Uchaguzi Songea mjini kuanzia Mei 2 hadi 4 mwaka huu.Mazoezi hayo ni uwekaji wazi wa daftari la kudumu la Mpigakura na uboreshaji wa daftari la kudumu la Mpigakura.
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.