Serikali mkoani Ruvuma imekemea na kuwaonya watumishi wa umma wanaofanyakazi maeneo ya mipakani kuacha kujihusisha katika vitendo vya rushwa ikiwemo kuwaruhusu wageni kuingia wakati wanatakiwa kuwekwa karantini kwa siku 14.Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme alikuwa anazungumza na watumishi wa Kituo cha Uhamiaji Mkenda Songea kilichopo mpakani mwa nchi ya Tanzania na Msumbiji.
WAZIRI Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema jumla ya watu 167 wamepona ugonjwa wa corona nchini Tanzania ambapo hadi sasa katika nchi nzima kuna jumla ya visa vya watu 480 vya corona.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas amezitaja hatua 40 ambazo zimechukuliwa na serikali inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli katika kukabiliana na virusi vya corona nchini.
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.