Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amefungua minada ya mazao kwa mfumo wa stakabadhi ghalani katika msimu wa mwaka 2019/2020.Minada hiyo itakuwa inafanyika katika wilaya za Songea, siku ya Jumatatu,Namtumbo siku ya Jumatano na Tunduru siku ya Alhamis .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 22 Aprili, 2020 amezungumza na Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama akiwa Chato Mkoani Geita kuhusu hali ya ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (Covid-19).Mhe. Rais Magufuli amewashukuru Watanzania kwa kuitikia wito wa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona, na kwa kushiriki katika siku 3 za kumuomba Mwenyezi Mungu aepushe janga la ugonjwa huo.
Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma kimeunga kwa vitendo jitihada za serikali za kupambana na virusi hatari vya Corona baada ya kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni tatu.
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.