Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme ameiomba benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania (TADB) kufungua tawi la benki hiyo katika mkoa huo pamoja na kuanzisha viwanda vya kuchakata mazao.Mndeme amesema kuwepo kwa benki hiyo kutawasaidia wakulima wa mkoa huo kukopa pesa na kuziingiza katika kilimo na kuwainua kiuchumi na uwepo wa viwanda kutasaidia kuongeza mnyororo wa thamani pamoja na kutoa fulsa ya ajira kwa wananchi wa Ruvuma.
MKUU wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema aliunda Tume ya kuchunguza migogoro ya ardhi katika Manispaa ya Songea.Akizungumza baada ya kupokea ripoti kutoka kwa Tume ametaja njia ambayo inaweza kupunguza migogoro ya ardhi katika Wilaya ya Songea na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.
SERIKALI ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli imetoa zaidi ya shilingi bilioni 37 kuboresha uwanja wa ndege wa Songea mkoani Ruvuma.
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.