Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amekagua mradi wa ujenzi wa zahanati ya Misufini Kata ya Luchili Halmashauri ya Namtumbo .Serikali imetoa shilingi milioni 50 kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo ambayo imejengwa kwa nguvu za wananchi
Mkuu wa Mkoa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amekagua miradi inayotekelezwa kwa force akaunti Wilaya ya Namtumbo ambapo ameagiza ni lazima wananchi washirikishwe pia taratibu za fedha zifuatwe .
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ameziagiza Halmashauri zote nane kupitia wataalam wa afya kusimamia kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya wimbi la tatu la corona.RC Ibuge ametoa maagizo hayo wakati anazungumza na wakuu wa wilaya,wakurugenzi wa Halmashauri na watumishi wa umma ngazi ya Mkoa na wilaya zote kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.