Waziri Mkuu Kassim Majaliwa yupo mkoani Ruvuma katika ziara ya kikazi ambapo Januari 5 mwaka huu asubuhi atazindua meli mpya ya abiria ya MV Mbeya II katika bandari ya mji wa Mbambabay wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajia kufungua jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Mji Mbinga na kukagua nyumba nane za Watumishi wa Halmashauri hiyo siku ya Januari 4 mwaka huu mjini Mbinga.
WAZIRI Mkuu Kasssim Majaliwa amesema sasa ni rasmi ndege ya kwanza ya abiria kupitia Kampuni ya ATCL inatarajia kutua katika kiwanja cha Ndege Songea Januari 15,2021.Waziri Mkuu ametoa ahadi hiyo kufuatia ombi la Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme alilolitoa wakati anatoa taarifa ya shughuli za maendeleo Mkoa wa Ruvuma katika siku ya kwanza ya ziara ya kikazi ya Waziri Mkuu Mkoani Ruvuma ambayo imeanza Janauri 2 hadi sita mwaka huu.
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.